Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Balozi Charlotta Ozaki Macias, muda mfupi baada ya kuwasili kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo mapema leo Jumatano Novemba 20, 2024.
Mhe. Balozi Charlotta licha ya kusaini kitabu cha wageni, amafanya makubalino na Mhe. Makonda akimuahidi kuendeleza mahusiano ya muda mrefu yaliyopo kati ya pande hizo mbili hasa katika kuwanufaisha wananchi wa pande hizo mbili kisekta.
Balozi Charlotta yuko mkoani Arusha akiwa ameambatana na wadau wa Shirika la Kimataifa kutoka Umoja wa Ulaya linalofadhili miradi ya Elimu (GPE) kwa lengo la kukagua utekelezaji na maendeleo ya miradi hiyo, iliyogharimu zaidi ya Bilioni 4 kwaajili ya kusaidia maendeleo ya sekta ya elimu katila mkoa wa Arusha
Hata hivyo Mhe. Makonda ameahidi kuhakikisha kuwa miradi hiyo inafanya kazi kama ilivyotarajiwa ya kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwenye miundombinu bora na rafiki muda wote ili kurahisisha tendo la kufundisha na kujifunzia.
Awali, GPE inaongozwa na Mwenyekiti wa bodi na Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete linatoa ufadhili wa elimu kwa wadau mbalimbali katika kuimarisha mifumo bora ya elimu kwa nchi zaidi ya 89 ikiwemo Tanzania, ambapo huyaweka pamoja mataifa yanayoendelea, wafadhili, mashirika ya kimataifa na sekta binafsi na Umma ili kusaidia uboreshaji wa Elimu kote duniani.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa