• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

BILIONI 88 ZATEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO NGORONGORO:  MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA..

Posted on: September 2nd, 2025

 _Rc Makalla apokelewa kwa shangwe, akifanya ziara yake Wilayani Ngorongoro


. Wananchi wamshukuru Rais Samia kwa miradi mingi ya maendeleo_

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla amefanya ziara ya Kikazi Wilayani Ngorongoro leo Jumanne Septemba 02, 2025, akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kwa kutoa zaidi ya Bilioni 88 kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo Wilayani humo, ikiwemo Bilioni 18.9 zinazotekeleza miradi 17 ya Maji kwenye Kata mbalimbali za Ngorongoro.


Mhe. Makalla ameyaeleza hayo mara baada ya kupokelewa Wilayani Ngorongoro na kuzungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, akimpongeza pia Mkuu wa Wilaya hiyo Brigedia Jenerali Wilson Christian Sakulo kwa kuongeza makusanyo kwenye sekta ya mifugo kutoka Shilingi Milioni 13 kwa mwaka hadi zaidi ya Milioni 200 na kusema fedha hizo zitasaidia kuongeza uwezo wa Halmashauri hiyo katika kuwahudumia wananchi.


"Wilaya ya Ngorongoro inapokea fedha nyingi, miradi mingi mfano ukichukulia tu sekta ya maji, Wilaya hii ya Ngorongoro ina miradi 17 ya maji inayotekelezwa kwa wakati mmoja na katika miradi hiyo ya Maji Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameleta fedha bilioni 18.9 kutekeleza miradi hiyo na Sale yenyewe ina mradi wa maji" amesema Mhe. Makalla.


Aidha katika salamu zake, Mkuu wa Mkoa mbali ya kuhimiza kushirikiana pamoja katika kuwaletea wananchi maendeleo na kutimiza maono ya Rais Samia katika kuwatumikia wananchi, amesisitiza umuhimu wa Viongozi wa Wilaya hiyo kuendelea kulinda na kudumisha amani na utulivu katika kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu ili kuruhusu wananchi kushiriki kikamilifu kwenye kampeni na uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.


Awali katika maelezo yake, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro ameeleza pia kuwa hali ya ulinzi na usalama katika Wilaya hiyo ni shwari na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo unaendelea vyema, akieleza pia kuhusu  uwezeshaji wa wananchi kiuchumi ambapo kwa mwaka 2024/25, Jumla ya shilingi Milioni 634 zimetolewa kwa vikundi 130 vya wanawake, Vijana na wenye ulemavu.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO MTIHANI WA UTAMIRIFU (MOCK) 2025 DARASA LA SABA (VII)- MKOA WA ARUSHA June 07, 2025
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKALLA: UFUNGUZI TAWI LA CRDB NAMANGA UTACHOCHEA BIASHARA NA UCHUMI WA WANANCHI WA MPAKANI ..

    September 26, 2025
  • RC MAKALLA ATAKA MPANGO MKAKATI WA UTALII UKIJUMUISHA FURSA NA MAANDALIZI YA AFCON 2027...

    September 25, 2025
  • WANANCHI WALIOLALAMIKIA MGAO WA MAJI WAFURAHIA UJENZI WA TENKI JIPYA LA MAJI...

    September 24, 2025
  • RC MAKALLA: ARUSHA ITAENDELEA KUWA NA AMANI SASA NA HATA  BAADA YA UCHAGUZI...

    September 24, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa