Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amewataka makarani wa sensa Mkoa wa Arusha kuwa makini, wenye nidhamu na uzalendo zaidi katika kazi ya sensa na inapotokea changamoto watoe taarifa mapema.
Ameyasema hayo, alipokuwa akizungumza na makarani hao katika vituo vya kutoa mafunzo ya sensa kwenye Jiji la Arusha na Halmashauri ya Meru.
Wanatakiwa wakawe makini zaidi kwenye zoezi la sensa ili kuweza kupata takwimu sahihi zitakazowezesha kupanga mipango bora kwa Mkoa wa Arusha.
Aidha, amesisitiza katika siku ya zoezi la sensa wakawe makini kwa kujiepusha na mambo yatakayovuruga utendaji wao wa kazi na hivyo kupelekea kuaribu kazi ya sensa kwa ujumla.
Amewataka kila mmoja akafanye vizuri kwenye eneo lake kwa kupata taarifa sahihi na hiyo inatasaidia kupata matokea mazuri kwa Mkoa mzima wa Arusha.
Nae, Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Musa amewataka makarani wa sensa kuyafanyia kazi mafunzo yote waliyopewa ili waweze kupata idadi sahihi ya watu na makazi.
Amesema makarani ni watu ambao wanategemewa sana katika zoezi hili hivyo kufanikiwa kwake ni fahari kwa Mkoa na kwao pia.
Kaimu Mratibu wa sensa bwana Jonas Mwita amesema jumla ya makarani 7807 wanapatiwa mafunzo maalumu ya sensa katika vituo 82 kwa Mkoa wa Arusha.
Mhe. Mongella pamoja na Katibu Tawala Mkoa bwana Missaile Musa wamefanya ziara ya kukagua mafunzo ya sensa kwa makarani wa Jiji la Arusha na Halmashauri ya Meru ili kufahamu changamoto wanazokumbana nazo katika mafunzo hayo.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa