Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Arusha kwa kuwasalimia na kuzungumza na wananchi wa wilaya ya Arumeru eneo la USA River, Mapema leo 04 Juni, 2024.
Katika Mkutano huo, Dkt. Nchimbi ametumia amesikiliza kero za wananchi, kero ambazo baadhi yake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amezitolea ufafanuzi na kuahidi kuendelea kutembelea wananchi kwenye maeneo yao ili kuwagikia na kutatua kero hizo.
Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo, amemtaka Mhe. Makonda kuendelea kufuatilia kero na matatizo ya wananchi kwenye maeneo yao ili kufikia malengo ya Serikali ya kuhudumia wannachi pamoja na kutatua kero zao.
Amewataka wananchi kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi na Serikali yake ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan, kutokana na kazi kubwa inayoifanywa ya kupelekea huduma za kisekta karibu na wananchi.
Awali, Dkt. Nchimbi amesimama eneo hilo akiwa njiani kutokea mjini Arusha mjini kuelekea Mji wa Bomang’ombe, Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro,tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo.
Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Balozi Nchimbi ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Komredi Amos Gabriel Makalla na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Hamid Abdalla.
#VitendoVinaSauti
#TunaendeleaNaMama
#KaziIendelee
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa