Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mhe.John V.K Mongella leo tarehe 26/07/2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Vietnam Nchini Tanzania Mhe. Nguyen Nam Tien.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Balozi Nguyen amelezea uhusiano mkubwa wa Kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Vietnam kuwa umedumu tangu mwaka 1965 mara baada ya Muungano wa Serikali ya Tanganyika na Zanzibar kuungana,huku akitabaibisha kuwa uhusiano huo ulijengwa zaidi ya Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere chini ya mfumo wa Siasa za Kijamaa.
Aidha,Balozi Nguyen aliendelea kueleza kuwa Vietnam imefurahishwa na Uongozi wa Rais Dkt Samia kwa kusimamia kwa dhati Siasa za Kiplomasia za Kiuchumi kwa kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na Mazingira mazuri na tulivu ya kiuwekezaji na kuhahidi kutumia fursa hiyo katika kuwaleta wawekezaji na wafanyabishara toka Vietnam kuja Arusha kwaajili ya kuangalia fursa mbalimbali zilipo.
Balozi Nguyen amesema kuwa Vietnam ni Nchi ya 40 katika ukuaji wa Kiuchumi Duniani na amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mhe.John Mongella kuwa Vietnam iko tayari kushirikiana Tanzania hususan Arusha katika kubadilishana utaalam mbalimbali ikiwemo maendeleo Viwanda na Teknolojia ya Mawasiliano kwani tayari Vietnam wanaendesha makampuni ya Mawasiliano ikiwemo Kampuni ya Simu ya HALOTEL.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella amemweleza Balozi Nguyen kuwa Arusha ina fursa rukuki zikiwemo Utalii,Kilimo,Mifugo na Viwanda hivyo kumwomba kuitangaza Arusha Nchini Vietnam kwa kuwaalika Wawekezaji toka Sekta mbalimbali kuja kuwekeza katika Mkoa wa Arusha kwani Mkoa Una mazingira mazuri ya kiuwekezaji na miundombinu inayorahisha shughuli za uwekezaji ikiwemo Viwanja vya ndege vya KIA,Reli ya Arusha kwenda Dar na barabara za uhakika zinazopitika majira yote ya Mwaka.
Aidha,Mhe.Mongella amemweleza Balozi kuwa Serikali ya Rais Dkt.Samia imeweka kipaumbele Kikubwa katika kuweka mazingira wezeshi kwa Wawekezaji kuja kuwekeza Nchi Tanzania hii imetokana na kusimamia vyema Sera ya Diplomasia ya Kiuchumi ambayo mpaka sasa Tanzania inaendelea kunufaika na Sera hiyo Duniani.
Vile vile Mongella amesema Arusha ni lango Kuu la Utalii kwani asilimia kubwa ya Watalii wanaingia Tanzania hupitia Arusha hivyo kutoa fursa kubwa kwa Wawekezaji toka Vietnam kuja kuwekeza katika Sekta ya Utalii kwa kuendesha biashara ya Hotel pamoja na Usafirishaji Watalii.
Balozi wa Vietnam Nchini Tanzania yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa