RC Mongella ametoa wiki mbili za kuhakikisha zoezi la usanifu wa mabwawa 2 ya Maji Monduli Juu unakamilika.
Ameyasema hayo alipokuwa akikagua mradi wa Maji Wilayani Monduli, ambapo mradi wa Maji wa Kijiji cha Enguiki umegharimu kiasi cha Bilioni 2.5 na mradi wa Kijiji cha NAFCO umegharimu zaidi ya Bilioni 1 zilizojenga visima vya Maji takribani 13.
Mpango wa Serikali ni kuhakikisha inamtua mama ndoo kichwani, hivyo wananchi wa Wilaya ya Monduli wasiwe na wasiwasi kwani Maji yatawafikia.
Aidha, amewasisitiza viongozi wa kata, Vijiji na madiwani kuhakikisha wanafuatilia uchimbaji wa visima hivyo katika maeneo yao na kusimamia vichimbwe kwa uhakika zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha amefanya ziara ya kukagua miradi ya Maji, Afya na Elimu katika Wilaya ya Monduli na kujionea namna fedha za Serikali zinavyotumika.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa