• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

ACHENI KUVAMIA MAENEO YA HIFADHI - RAIS SAMIA

Posted on: July 13th, 2024


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kuacha kuvunja sheria kwa kuvamia maeneo ya hifadhi na badala yake kutunza mazingira hayo.


Kauli hiyo imekuja kutokana na maombi ya Mbunge wa Mlele, Mhe. Isack Kamwelwe aliyeomba kumegewa ardhi katika maeneo ya hifadhi ya mapori yaliyopo jimboni kwake.


Ameyasema hayo leo Julai 13,2024 alipokuwa akizungumza na wananchi katika Wilaya ya Mlele, Kata ya Inyonga Mkoani Katavi.


"Tunajua kuna uhaba wa Ardhi na kuna maeneo ya hifadhi mnayatamani lakini hayaendani na kuvunja sheria tukae tuzungumze tuangalie namna ya kuyamega na si kuvamia" amesisitiza Mhe. Rais Samia.


Awali, akitoa ufafanuzi kuhusu ombi la Mhe. Kamwelwe  la kuongezewa hekta elfu 15 katika Pori la Akiba Inyonga,Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amesema kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii imepokea maombi hayo na inaendelea kufanya tathimini kuangalia uhitaji halisi na kuyawasilisha kwa mamlaka kwa hatua zaidi.


Amefafanua kuwa mwaka 2021  uamuzi wa Baraza la Mawaziri ulitoka ambapo hekta elfu kumi zilipunguzwa kwa ajili ya wananchi wa Kijiji cha Kamsisi.


Katika hatua nyingine Mhe. Kairuki ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wa Inyonga kuendelea kushirikiana na Serikali katika utunzaji wa mazingira, misitu na kuhakikisha hakuna uvamizi katika mapori.


Pia amewapongeza wananchi wa Katavi kwa kuwa na jitihada katika shughuli za ufugaji nyuki ambapo kuna wafugaji zaidi ya 2132 ambao wamewezesha kupatikana kwa zaidi ya shilingi bilioni 21.5.


Mkutano huo pia umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi.


Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA AFUNGUA MKUTANO WA 33 WA WAKUU WA MAJESHI YA ULINZI (SADC).

    May 30, 2025
  • SAMIA MOTOCROSS CHAMPIONSHIP KUREJEA MSIMU WA PILI JULAI 12, 2025

    May 27, 2025
  • MKOA WA ARUSHA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUBWA WA WAKUU WA MAJESHI WA SADC

    May 25, 2025
  • UJENZI WA UWANJA WA AFCON ARUSHA SIO MICHEZO TU, NI FURSA YA KIUCHUMI

    May 24, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.