“Amani, Utulivu na mshikamano ni matokea chanya ya kuwa na nchi yenye dini zilizo imara katika kuombea hivi vitu”.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, alipokuwa akizungumza na waumini wa kanisa la Safina jijini Arusha.
Amesema kutokana na maombezi ya waumini wa dini zote ndio maana nchi ya Tanzania imeweza kushinda vita mbalimbali vikiwemo vya uvamizi wa wadudu aina ya Nzige na ugonjwa wa Corona.
Amewataka watanzania wote kuendelea kuiombe nchi yetu na pia kuombea viongozi watakaorudi kwenye madaraka wakawe viongozi wenye hofu ya Mungu na wapenda kutenda haki.
Aidha, amewahimiza waumini wote kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi na kuchagua viongozi watakaependa maendeleo ya nchi na kuwa viongozi bora.
Akitoa salamu za Mkoa wa Arusha kwa niaba ya wananchi wote, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Iddi Hassan Kimanta, amesema wana Arusha wanaishi kwa kumtegemea Mungu kwa kila kitu.
Pia, amewahasa wananchi wa Arusha kuto kukubali kugombanishwa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.
Amewataka wana Arusha wajitokeze kwa wingi siku ya uchaguzi na kuchagua viongozi watakao waletea maendeleo.
Waziri Mkuu amehitimisha ziara yake ya kampeni za uchaguzi Mkoani Arusha kwa kufanyiwa maombi maalumu katika tamasha la maombi lililoandaliwa na kanisa la Safina Jijini Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.