Imeelezwa kuwa Mkoa wa Arusha una Mkuu wa Mkoa Hodari ambaye kwa kipindi kifupi alichokaa Arusha, licha ya juhudi zake za kazi za maendeleo ya kiuchumi na kijamii, amekuwa mstari wa mbele katika kuwasemea na kutatua kero za wananchi wa Mkoa wake wakati wote.
Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa, wakati akuzungumza kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Kilombero Jijini Arusha, ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi mkoani Arusha Oktaba 04,2024.
Mhe. Mchengerwa amewataka wananchi wa mkoa wa Arusha kujikita kwenye ujenzi wa Taifa kwa kushirikiana na viongozi wote wa mkoa huo chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa wao Mhe. Paul Christian Makonda @baba_keagan,katika kuharakisha maendeleo ya mtu mkoja mmoja na mkoa kwa ujumla wake.
Amewataka wananchi wa Arusha kutoendekeza siasa badala yake kufanyakazi kwa bidii na kuwaomba kushirikiana na Mkuu wa Mkoa katika kuharakisha maendeleo ya mkoa wao.
"Makonda chapa kazi asikutishe mtu, Unashughulika na waliodhulumiwa, unashughulika na Maskini, unashughulika na yatima, unashughulika na wajane na Hii ndiyo kazi uliyotumwa na Rais Samia Suluhu Hassan. Chapa kazi, Mhe. Rais anakuamini sana, Waziri wako nakuamini achana na siasa za majitaka za mitandaoni." Amesema Mhe. Mchengerwa
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.