Arusha Imependelewa na Mama Samia Suluhu Hassan amekoleza Upendeleo huo kwa Kuutangaza Utalii wa Arusha kote duniani kupitia filamu aliyoamua kuingoza mwenyewe ya The Royal Tour pamoja na filamu ya Amazing Tanzania, Filamu zilizoongeza maradufu idadi ya watalii na wageni wanaofika Jijini Arusha Usiku na Mchana kuja kushuhudia Uumbaji na Upendeleo Mkubwa wa Arusha.
Wakati huu msisimko umekuwa ni mkubwa zaidi Chini ya Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Christian Makonda ambaye pamoja na mengine mengi, Kazi kubwa aliyoagizwa kuifanya Arusha na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imekuwa ni kuukuza utalii wa Arusha.
Tayari Kazi kubwa inafanyika na Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema Arusha Inarudi kwenye ramani ya dunia katika Utalii kwa kuhakikisha matukio yanakuwepo ya Kutosha Arusha na Arusha inakuwa chaguo namba moja la Watalii wanaokuja kutalii kwenye bara letu la Afrika.
_Kazi Iendelee_
_Arusha kwenye Viwango vingine_
_ArushaNaUtalii_
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.