Na Prisca Libaga Arusha
Serikali ya awamu ya sita imesisitiza kwamba itaendelea kuboresha Miundombinu ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii ya Tengeru (TICD) iliyopo Mkoa wa Arusha, wilaya ya Arumeru, kwa lengo la kukipa uwezo wa kutoa mafunzo kwa wataalamu vijana na kufikia malengo ya serikali ya kuwahudumia na kuchochea maendeleo kwa wananchi, hususani wa ngazi ya chini ya vijiji na katika vitongoji
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Anastaz Mpanju ametoa mwelekeo huo wakati wa kongamano la kitaaluma kuelekea kilelele cha maadhimisho ya miaka 60 ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo yenye umahiri kwenye kada ya Maendeleo ya Jamii Tanzania.
Naye Mkuu wa Tasisi hiyo Dkt. Bakari George ameeleza namna Serikali ilivyoiboresha taasisi hiyo ambayo awali ilifahamika kama Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru
Kwa upande wao wanafunzi wa taasisi hiyo wanaeleza matarajio yao ya kuibua na kutatua changamoto kwenye Jamii.
Mwisho
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.