• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

BARABARA YA MIANZINI-NGARAMTONI YAMEKWA JIWE LA MSINGI

Posted on: May 19th, 2023

"Ujenzi wa Barabara ya Mianzini hadi Ngaramtoni yenye urefu wa kilomita 18 itafungua fursa mbalimbali za maendeleo ikiwemo kurahisisha usafiri kwa wananchi".

Yamesemwa hayo na Makamu wa Raisa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango baada ya kuweka jiwe la msingi katika barabara hiyo eneo la Ngaramtoni ya juu.

Amesema,Serikali imewekeza fedha nyingi katika miundombinu ya barabara ili kuwarahisishia wananchi katika shughuli zao za kiuchumi.

Pia, Dkt. Mpango amewataka askari wa usalama barabara kuisadia serikali kusimamia sheria za usalama barabarani kihalali ili kupunguza vifo vya watu na hata wengine kuachwa wakiwa walemavu wa viungo.

Vilevile, amewahasa madereva wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani, ili waweze kulinda uhai wao.

Dkt. Mpango amesema juhudi za serikali zilizofanywa hadi sasa katika bajeti ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ilikuwa bilioni 275  mwaka 2022/2023 ilikuwa bilioni 771.8 na bajeti tarajiwa  ya 2023/2024 inakadiriwa kuwa bilioni 818.02.

Amesisitiza juhudi hizo ni kuwawezesha TARURA kuhudumia vizuri mtandao wa barabara kwa ukubwa.

Kwa Mkoa wa Arusha, TARURA wamepatiwa bilioni 19.5 kwa bajeti ya mwaka 2023/2024 na hii itasadia kurekebisha zaidi barabara zote hata zile zilizoharibiwa na mvua.

Aidha, amewataka wananchi wakatunze  mazingira kwa kuacha kukata miti hivyo na kuwataka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kupanda miti ya vivuli na Matunda katika barabara hiyo ili iweze kupendeza zaidi.

Akisoma taarifa kwa ufupi, Naibu Waziri wa ujenzi na miundombinu Godfrey Kasekenya amesema fidia ambayo itatolewa ni kwa wale wananchi wa barabara kuanzia Olemringaringa hadi Ngaramtoni na wale wananchi wa Mianzini hadi Ngaramtoni hawatalipwa kutokana na kanuni na  sheria za barabara.

Nae,  Mtendaji wa TANROADS Mhandisi  Logatius Matibila amesema barabara hiyo ya kilometa 18 itagharimu bilioni 22.2 bila kodi ya ongezeko la thamani (VAT) hadi kukamilika kwake.

Amesema mkataba wakuanza ujenzi ulisainiwa  Januari 19, 2022 na ujenzi ulianza Mei 20,2022 na unatarajiwa kukamilika Agosti 2023.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amesema Serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeleta fedha nyingi katika sekta mbalimbali ikiwemo ya miundombinu ya Barabara na kuwezesha Mkoa kuendelea kuboresha barabara zake ili ziwe rahisi kupitika.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango amemaliza ziara yake ya kikazo ya siku 4 kwa Mkoa wa Arusha na ameridhishwa na miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa katika Mkoa wa Arusha hususani aliyoipitia na kuwataka wananchi waitunze kwani fedha nyingi zimetumika kuijenga ambazo ni kadi zao.


Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.