Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ameuagiza Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kutumia fedha za mapato ya ndani shilingi Bilion 2.1 kujenga barabara ya Esso - Longdon iliyopo kata ya Sokoni I na Unga Ltd jijini humo.
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa ziara yake Jijini humo na kutembelea barabara ha Esso - Longdon na kuona umuhimu wa barabara hiyo kujengwa kwa kiwango cha Lami.
Mhe. Mchengerwa alisema hakuna haja ha Jiji kuwa na fedha kwenye Akaunti zenu wakati wananchi wanahitaji huduma bora sasa nawaeleleza tumieni fedha za mapato ya ndani.
Aidha aliwalekeza kuzungumza na wananchi walioko pembeni na barabara hiyo ambao wataathiriwa na mradi kuona namna bora ya wao kupisha ili kutoa fursa kwa barabara hiyo kujengwa kwa kiwango cha Lami na kuongezewa thamani.
Barabara ya Esso - Longdon ina urefu wa Km 1.8 na inapita kwenye Kata mbili ya Unga Ltd na Sokon 1 jijini Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.