Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amewataka wakuu wa shule za Korona na Makiba kwenda kusimamia ujenzi wa miundombinu ya shule zao kwa kufuata waraka uliotolewa.
Ameyasema hayo alipokuwa akiwasainisha mikataba Wakuu wa Wilaya ya Arusha na Arumeru kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba vya Madarasa 19, Mabweni 7 na Matundu ya Vyoo 28 yatayojengwa katika shule ya Korona iliyopo halmashauri ya Jiji la Arusha na Makiba halmashauri ya Meru.
Mongella amesema, Mkoa hautaruhusu ubora wa majengo upungue kutokana na kuyumba kwa usimamizi.
Amesema ujenzi wa miundombinu hiyo ukamirike ndani ya siku 90 kuanzia mwezi Mei na Wakuu wa Wilaya wakasimamia kwa ukaribu zaidi.
Aidha, fedha zaidi ya bilioni 1 zimepokelewa kwa ajili ya ujenzi huo na umegawanywa kwa shule ya Sekondari Korona zaidi ya Milioni 800 na shule ya Sekondari Makiba zaidi ya Milioni 615.
RC Mongella amesisitiza kuwa katika miradi hiyo ni fursa kwa kila mtu kuthiririsha uzalendo wake, weredi na nidhani katika kazi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.