BUNGE LAPITISHA TRILIONI 10.125 OFISI YA RAIS - TAMISEMI
OR- TAMISEMI
BUNGE limeidhinisha matumizi ya Shilingi trilioni 10.125 kwa ajili ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI, sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi zake kwa mwaka 2024/25 na kati ya hizo Sh trilioni 3.415 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Fedha hizo zilizoidhinishiwa na bunge zimeongezeka kwa takribani sh bilion 900 ikilinagnishwa na bajeti ya Sh. triloni 9.18 zilizoidhinishwa mwaka 2023/24.
Pia Bunge limeidhinishia Ofisi ya Rais - TAMISEMI, taasisi zilizo chini yake, mikoa 26 ikijumuisha halmashauri 184 kukusanya maduhuli na mapato ya ndani ya Sh trilioni 1.60.
Aidha, katika fedha zilizoidhinishwa Sh bilioni 17.79 zinaelekezwa kwa ajili ya kuratibu na kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024.
Pia Sh trilioni 1.02 zitatumika katika kutekeleza shughuli katika sekta ya elimu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.