Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake itatatua changamoto zote za wananchi hivyo wasiwe na wasiwasi.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kikatiti Wilaya ya Arumeru.
Changamoto za Barabara, Maji na kituo cha Afya Kikatiti vyote vitafanyiwa kazi.
Katika kuendeleza Zahanati ya Kata ya Kikatiti Mhe. Rais Samia Saluhu ametoa shilingi Milioni 10 zakusaidia kuboresha kituo hicho ili kiweze kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amewasili Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku 2 ambapo atatembelea mradi wa Maji wa Chekeleni, atazindua hospitali ya Wilaya Jiji la Arusha na kuzungumza na wananchi katika kiwanja cha Sheikh Amri Abeid. Kisha atazindua kiwanda cha Nyama Longido, uzinduzi wa mradi wa Maji Longido na atafanya Mkutano wa hadhara stendi mpya Longido.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.