Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda akitoa salamu za Mkoa wa Arusha kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo, wakati wa Mkutano wa 21 za Taasisi ya Fedha, unaofanyika kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha (AICC) Ukumbi wa Simba jijini Arusha, leo Machi 7, 2024.
Mhe. Emmanuela ametumia fursa hiyo kuwashukuru waandaaji wa mkutano huo, Benki Kuu ya Tanzania na Jumuiya ya Umoja wa Mabenki nchini, kwa kuichagua Arusha kufanyika Mkutano huo wa 21, mkutano ambao amekiri kuwa muhimu sana kwenye sekta ya fedha.
Aidha amemshukuru Makamu wa Rais, Mhe. Dkt.Isdori Mpango kwa jitihada kubwa zinafanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hasani za kuchochea maendeleo ya sekta ya fedha na ukuaji wa uchumi nchini.
Mkutano huu unadhihirisha vipaumbele vya serikali katika kuweka mazingira wezeshi ya kuimarisha ukuaji wa uchumi, ikiwemo sekta ya fedha, hasa nyakati zenye changamoto za kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kuweka sera nzuri na shirikishi zitakazofanya sekta binafsi ikue vile vile" Ameweka wazi Mkuu wa wilaya huyo.
Hata hivyo, hakusita kuwakaribisha wageni wetu wote mkoa wa Arusha, ambo ni kitovu cha utalii nchini, na kuwasihi watumie wakati huo kujionea na kufurahia vivutio mbalimbali vilivyopo kama Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ambayo ambayo ni sehemu ya urithi wa dunia, Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Mlima Meru na Oldonyo Lengai, kilimo cha bustani na matunda, uoto wa asili, hoteli za kitalii pamoja na tamaduni za makabila mbalimbali yanayopatikana kwenye mkoa wetu wakiwemo Wamaasai.
Mkutano huo wa siku mbili, ulioandaliwa Benki Kuu ya Tanzani kwa kushirikiana Benki na Jumuiya ya Umoja wa Mabenki, Mada kuu ikiwa ni Kuimarisha Ustahimilivu wa Sekta ya Fedha Nyakati za Changamoto za Kiuchumi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.