Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, amewataka wanawake kununua bidhaa zinazotengenezwa na wanawake wenzao ili kuwaunga mkono, katika mapambano ya kujiinua kiuchumi.
Mhe. Kaganda ameyasema hayo wakati alipotembelea na kukagua mabanda ya Maonesho ya Biashara za Wajasirimali, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani, yaliyofanyika kwenye, viwanja vya Ngarenaro, Jijini Arusha.
Amesema kuwa, wanawake wanajitahidi kutengeneza bidhaa bora zinazotokana na rasilimali zinazopatikana nchini, bidhaa ambazo ni bora kwa afya, hivyo wanawake wanahitaji kuungwa mkono na watanzania wote hususani kundi kubwa la wanawake.
"Wanawake tuwe mstari wa mbele kununua bidhaa zinazotengenezwa na wanawake wenzetu, tuanze sisi wenyewe kununua bidhaa za wanawake wenzetu, tuwaunge mkono ili kuinuana" Amesema Mhe. Emmanuela
Hata hivyo amewasisitiza wanawake wajasiriamali kuhakikisha wanasajili biashara zao pamoja na kuweka bacon bidhaa zao, ili ziweze kuingia kwenye masoko rasmi ya ushindani na sio kutengeneza bidhaa zisizotambulika jambo ambalo linapoteza hadhi na kupotea sokoni kwa haraka.
Kauli Mbiu ni "Wekeza kwa Mwanawake ili Kuharakisha Maendeleo ya Taifa Pamoja na Ustawi wa Jamii"
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.