Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amewasili Jijini Arusha kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro leo Septemba Mosi, 2024, tayari kwaajili ya kufungua Jukwaa la 24 na mkutano wa 35 wa Kamati ya kudumu ya fedha ya Mkataba wa umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi.
Mkutano huo unafanyika kuanzia Septemba 02- 06, 2024 kwenye kituo cha kimataifa cha mikutano AICC ikiwa pia ni mara ya kwanza kwa mkutano huo kufanyika nchini Tanzania ikiwa ni maandalizi ya mkutano wa Cop29 unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu huko Baku nchini Azerbaijan.
Kwenye uwanja wa ndege wa Kilimanjaro, Mhe. Makamu wa Rais amepokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali na wa Chama Cha Mapinduzi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.