Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Akson amewataka watanzania, kujifunza kutokana na maisha mema na utumishi uliotukuka aliofanywa na hayati Edward Lowassa katika uhai wake.
Dkt. Tulia ameyasema hayo, wakati akitoa salamu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa ibada ya mazishi ya Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Lowasa, yaliyofanyika Kijiji cha Ngarash wilaya ya Monduli.
Amesema kuwa, kutokana na shuhuda njema zinazotolewa na watu mbalimbali juu ya utumishi wa Lowassa katika nafasi na nyadhifa mbalimbali alizoiztumikia, zinatuonyesha ni namna gani aliwekeza nguvu, juhudi na maarifa kulitumikia taifa na jamii yake
"Mimi sijawahi kufanya kazi na Lowassa, lakini amewahi kufanyakazi bungeni, sehemu ambayo ninaitumika sasa, na nimekuta alama za kazi zake alizozifanya zinazodhihirisha haya yanayosemwa na watu leo, kuwa alifanya mambo makubwa sana"
Amesisitiza kuwa, kutokana na maandika matakatifu kutoka kitabu cha Ayubu 14: 11, siku za mwanadanu si nyingi na huchanua na kunyauka kama maua, hivyo kila mwanandamu anapaswa kutumia vizuri muda aliyotunukia hapa duniani kwa kujipima kama ua lenye harufu nzuri amu mbaya.
Aidha amesisitiza Wagalatia 6:7, unaosema, msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna, tujiulize katika maisha yetu tumepanda nini katika dhamana tulizopewa za kuwahudumia wananchi ili siku moja watu waje kuushuhudia utumishi wako kwa jamii na Taifa.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.