Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt.Dotto Mashaka Biteko, amewaagiza wataalamu wanaohusika na ufuatiliaji na tathimini za utendaji wa Serikali kuzifanyia kazi Ripoti zote ili kuongeza ufanisha katika utendaji.
Kauli hiyo ameizungumza alipokuwa akifungua Kongamano la Kitaifa la ufuatiliaji, tathimini na mafunzo kwa taasisi mbalimbali za Serikali, Jijini Arusha.
"Mtu asiyejifanyia tathimini anakuwa ameduwaa tu wakati wote na anakuwa mtu wa hasara maana anakosa mwelekeo wa mambo yake",alisema.
Kongamano hilo litaisadia Serikali kujiwekea malengo yanayotekelezeka na kwa wakati.
Vilevile Serikali inatasaidia kubaini changamoto zinazoikabili Serikali na Taifa kwa ujumla na hivyo kurahisisha utatuzi wake kwa haraka.
Akisisitiza zaidi Mhe Biteko ametaka kuanzishwa kwa mfumo wa ufuatiliaji na tathimini wenye kuleta uwiano ambao utaende sambamba na sera yake kwa ufanisi ulio bora zaidi.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama amesema mada zitakazozungumziwa katika Kongamano hilo zitachochea maswala ya Utawala bora,TEHAMA na kuongeza uwazi wa utendaji wa Serikali.
Nae, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt.Jim Yonazi amesema Kongamano hilo limejimuisha takribani washiriki 524 kutoka taasisi mbalimbali za Serikali.
Lengo kubwa la kongamano ni kuwajengea uwezo, kujifunza na kufuatilia matokeo kwa njia sahihi huku wakichambua utendaji kazi wa Serikali.
Kongamano la Kitaifa la ufuatiliaji, tathimini na Mafunzo linafanyika kwa siku 3 Jijini Arusha na linatarajiwa kufungwa rasmi Septemba 14,2023.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.