Halmashauri za mkoa wa Arusha, zimesisistizwa kutenga fedha kwenye bajeti zao za mwaka kwa ajili ya kuchangia mfuko wa Afya wa Taifa, ili kutekeleza programu ya huduma ya usafiri wa dharura na rufaa kwa wajawazito na watoto m-mama.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Albano Musa, wakati akifungua kikoa kazi cha mwaka 2023/2024 cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mfumo wa m-mama mkoa wa Arusha, kilichofanyika kwenye hoteli ya Corridor Spring Julai 30,2024
Amewataka wakurugenzi wa halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya program ya M-mama, programu ambayo ni mkakati wa Serikali wa kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga, inayotoa huduma za usafiri bure kwa wajawazito na wazazi kutoka kwenye maeneo yao mpaka kufikia kwenye vituo vya afya kupitia namba 115.
Kufuatia taarifa ya tathmini iliyowasilishwa licha ya kupunguza vifo 19 kutoka vifo 64 mpaka kufikia vifo 48 sawa na 28%, zipo halmashauri ambazo hazijawalipa madereva waliofanya kazi hiyo angali wana mkataba wa kufanya kazi hiyo na kuwasisitiza kuhakikisha madereva hao wanalipwa fedha zao.
"Ni agizo la Serikali kila halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya kuendesha programu ya m-mama na kuhakikisha madereva wanaosafirisha wagonjwa wanalipwa kwa wakati, hakuna sababu ya kulimbikiza madeni yao, programu hii inachangia mafanikio ya Jamii, Serikali na agenda ya Mhe. Rais, hilo halitakubalika hata kidogo, tukusanye mapato tuchangie mfuko huo wa Taifa ili hata mdau akimaliza muda wake m-mama iwe endelevu".Amesisitiza RAS
Aidha amewataka waratibu wa m-mama kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili waifahamu vema huduma hiyo, na kufikia malengo ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuondoa vifo vyq wajawazito na watoto nchini na kuongeza kuwa, kupitia huduma ya m-mama huduma ambayo licha ya kuwa ni faraja kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Kwanza zaidi inaboresha maisha na ustawi wajamii ya watanzania.
"Ninaamina huduma ya m-mama ikiboreka inaweza kwenda mbali zaidi ya kuwahudumia watu wote zaidi ya wajawazito na watoto na kuokoa maisha ya watanzani wengi hasa waishio maeneo ya pembezoni"
Awali, kikao hicho kimewakutanisha watalamu wa sekta mtabuka ikiwemo wakuu wa Seksheni na Vitengo sekretarieti ya mkoa, makatibu Tawala wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, watalamu wa sekta ya afya, wanasheria na wahasibu wa afya wa halmashauri zote za mkoa wa Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.