Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma amewakata viongozi wa Mkoa wa Arusha kuhakikisha wanafuatilia maboresho yanayofanywa na Mahakama katika Mkoa wa Arusha.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na kamati za maadili ya mahakama ya Mkoa na halmashauri zote za Mkoa wa Arusha.
Amesema Mahakama kwa sasa inaendelea kufanya maboresha ya mfumo wake wa utendaji hasa baada ya kupata maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi.
Aidha, amesema wananchi wanapaswa kuyafahamu maboresho hayo ili wapate uwelewa zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Iddi Hassan Kimanta, amesema wajumbe wa kamati hizo wanatakiwa wajifunze zaidi namna ya uwendeshaji wa kamati hizo.
Amesema majukumu ya kamati hizo ni kusimamia maadili ya Mahakimu kwa kufuata taratibu katika nyanja mbili, za kazi na nje ya kazi ili kuongeza ufanisi wao.
Kimanta amesema baada ya kikao hicho kilichopanua uwele zaidi kwa wajumbe wa kamati hizo, hivyo wataenda kusimamia haki katika utendaji wao.
Tume ya utumishi wa mahakama iliyo chini ya Jaji Mkuu ipo katika Mkoa wa Arusha kwa lengo la kukutana na wajumbe wa kamati za maadili kwa ngazi ya Mkoa na halmashauri na kukagua miundombinu ya Mahakama katika Mkoa wa Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.