Jamii imetakiwa kuwajali na kuwapa msaada watu wenye changamoto za afya ya akili, kwa kuwaelekeza sehemu sahihi wanazoweza kupata matibabu sahihi badala ya kuwanyanyapaa hali inayowasababishia matatizo zaidi na ongezeko la watu wenye taafya ya akili kwenye jamii zetu.
Rai hiyo imetolewa na Mganga Mkuu Mkoa wa Arusha Dkt. Charles Mkombachepa, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda kwenye mdahalo maalum wa kuhamasisha wananchi kutambua umuhimu wa afya ya akili, sababu za matatizo ya afya ya akili, changamoto na sehemu sahihi ya kupata huduma, mdahalo uliofanyika kwenye viwanja vya Jimkana baada ya matembezi ya hiari.
Dkt. Mkombachepa emeeleza kuwa, tatizo la afya ya akili bado ni changamoto kubwa Nchini, hivyo kila mawnajamii analo jukumu la kuchukua tahadhari ya kujilinda na kuwasadia wale ambao tayari wanapitia changamoto hizo.
“Nitoe rai kwa wananchi wote kutowanyanyapaa na kuwatenga watu wanaopitia changamoto za afya ya akili, kwa kuwaita majina ambayo yanawafanya wajisikie vibaya na kuhisi kukosa msaada, kwa kufanya hivyo kunasababisha kujisikika vibaya pamoja na ongezela kubwa la watu wenye matatizo ya afya ya akili kwenye jamii zetu.” Amesisitiza.
Naye Mkurugenzi wa ASAS ya kiraia, Julieth Kiwaga ameiomba Serikali kutenga bajeti ya kujenga vituo maalum vya kutoa kwa watu wanaopitia changamoto hizo,sambamba na kuandaa mitaala ya kutoa elimu shuleni ili kila mwanajamii kuwa na ufahamu juu ya changamoto za afya ya akili.
Hata hivyo, Daktari wa afya ya akili Mkoa wa Arusha Dkt. Charles Migunga, amezitajwa sababu za mtu kupata ugonjwa wa afya ya akili ni msongo wa Mawazo, mtindo wa maisha, kurithi kutoka wazazi, changamoto za maisha na wakati mwingine kusababisha kujiingiza kwenye uraibu wa dawa za kulevya.
Aidha, ameibainisha mikakati ya Serikali katika kukabiliana na changamoto hizo, ni kuendelea kutoa elimu kwenye makundi mbalimbali ikwemo wafanyakazi, vijana na wanafunzi ili kuwajengea uwezo wa kutambua kuhusu changamoto hizo..
Awali, takwimu za WHO zinaonyesha kuwa mtu mmoja kati ya nane anakabiliwa na changamoto ya Afya ya akili duniani.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.