Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Hassan Suluhu ameupongeza Umoja wa Posta Afrika kwa kuleta kichocheo cha maendeleo barani Afrika katika kuimarisha uchumi na kuutaka umoja huo kutumia mfumo mmoja wa utoaji huduma za maduka mtandao.
Rais Samia aliyasema hayo Jijini Arusha wakati akizundua jengo la kisasa lenye ghorofa 17 la Umoja Posta Barani Afrika ambalo litakuwa likitoa huduma mbalimbali yakiwemo Maofisi,kumbi za Mikutano pamoja na shughuli za biashara ikiwemo Migahawa mikubwa.
Rais Dkt.Samia amesema tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Posta Barani Afrika, Serikali imechukua hatua mbalimbali kwa kuipitia sera yake ya maendeleo ya Posta ikiwemo kubuni huduma mbadala.
"Posta ina nafasi kubwa sana katika maendeleo ya Nchi ikiwemo utengenezaji wa mfumo wa anuani za makazi kwa Mitaa kupewa majina"
Anuani milioni 12,700 ziliweza kukusanya ikiwemo mfumo wa Napa kwa baadhi ya Taasisi zimeanza kuutumia mfumo huo ikiwemo mfumo wa Utoaji Huduma mbalimbali kutumia One Stop Border.
Aidha,alisema matumizi ya Biashara Mtandao yanaenda kwa kasi kwa kushirikiana na sekta binafsi hivyo ni lazima sasa Posta ijikite zaidi katika kuleta mapinduzi ya kieletroniki.
Vile vile Dkt.Samia alisisitiza umoja huo kutumia zaidi mashirika ya ndani ya ndege badala ya kutumia mashirika ya nje kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanayajengea uwezo wa kujiendesha kifaida hasa kwa kutumia mfumo mmoja wa wautoaji huduma za maduka mtandao.
Akitoa historia ya maendeleo ya Mawasiliano Dunia, Dkt.Samia alisema miaka ya zamani mawasiliano yalikuwa yakifanyika zaidi kwa njia ya mdomo pia kupitia njia ya kuwatuma wanyama na kufikia karne ya 18 mawasiliano yalainza kupitia huduma za Posta kwa njia ya baharini,magari ili kufikisha barua.
Aidha,Dkt.Samia alisema mafanikio ya umoja wa Posta Afrika na hatimaye kuwa na Jengo kubwa ambalo limezinduliwa ni matunda ya utekelezaji wa ndoto za Viongozi wa Wakuu wa Afrika wakiwemo kina Mwl.Julius Kambarage Nyerere, Kwame Nkrumah na kina Kenneth Kaunda na ndoto hiyo imetimia kwani Umoja huu unaendelea kuimarika zaidi.
Awali ,Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema uzinduzi wa jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU) unamaanisha mageuzi ya kidigitali katika utoaji wa huduma za Posta barani Afrika.
Waziri Nape alisema wao kama Mawaziri wa Kisekta toka Nchi wanachama watahakikisha wanaweka vipaumbele vya kuimarisha umoja wa Posta Afrika kwaajili yakongeza kasi ya maendeleo Barani Afrika.
"juzi kulikuwa na Jukwaa la Viongozi Mawaziri wa Utoaji Huduma za Posta Barani Afrika,lenye tija na alisisitiza kuendelea kushirikiana na mawaziri wengine katika kuiamrisha njia za ushiriki wa sekta binafsi katika kukuza sekta hiyo".Alisema Waziri Nape
Waziri Nape alisema ni wakati wa Nchi za Bara la Afrika kufanya biashara na kushikamana kwa pamoja na hakuna sababu kwa Nchi za Afrika kuendelea kubaki maskini kwani kupitia umoja huo wa Posta ambao waasisi walitumia kama chombo cha ukombozi wa Nchi nyingi za Afrika Kisiasa hivyo adhma ile ile itumike kulikomboa bara la Afrika kiuchumi
Alisema Shirika la Posta kwa kaushirikiana na PAPU wamechapisha stempu kwaajili ya kutumika katika barua na zinaonyesha aina mbalimbali za stempu katika nchi za Afrika kwa ajili ya kulitangaza jengo la umoja huo pamoja na vivutio mbalimbali vya Utalii vinavyopatikana Barani Afrika.
"Posta imefanya mageuzi makubwa kutoka kuwa sehemu ya kutuma barua na sasa kuwa ya kidigitali zaidi na stempu hizo zitaenda kuitangaza nchi za PAPU Dunia nzima"
Aidha, Nnauye alisema kwa dunia ya sasa Posta inaenda kuwa sehemu ya kutuma na kupokea mizigo ya aina yote na ndiomaana serikali iliamua kutekeleza utoaji wa postcode nchi nzima.
Huku Katibu Mkuu wa Umoja huo,Sifunde Chief Moyo alishukuru jengo hilo kujengwa nchini Tanzania kutokana na Tanzania kuwa mstari wa mbele katika ukombozi wa Nchi nyingi za kusini na akaongeza kwa kusema kuwa ukiwa ndani ya Jengo hilo unaona Mlima Mkubwa Barani Afrika ,Mlima Kilimanjaro na Mlima Meru hivyo jengo hilo litaleta chachu ya ushirikiano kwa nchi za PAPU.
Huku Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella alimshukuru kujengwa kwa Jengo hilo ambalo linaongeza uzuri wa madhari ya Jiji la Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.