Na Elinipa Lupembe
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru amezindua Mradi wa Ujenzi wa vyumba 2 vya Madarasa na Ofisi, shule Kongwe ya Msingi Engikaret Kata ya Engikaret uliojengwa na Serikali kwa gharama ya shilingi milioni 50 kupitia programu ya BOOST.
Katika mradi huo, Ndugu Mnzavatoa jumbe za Kudumu za Mwenge wa Uhuru, kwa kuwahamasisha
Wananchi wenyz sifa kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika Oktoba 2024, kwa kusisitiza kuwa kila mwananchi anapaswa kutambua kushiriki uchaguzi na haki Kikatiba.
Ameitaka jamii kuongeza Mapambano dhidi ya Magonjwa ya kuambukiza ikiwemo ugonjwa wa UKIMWI kwa kuzingatia kauli mbiu Jamii iongeze kutokomeza UKIMWI na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria chini ya Kaulimbiu ya Ziro Malaria inaanza na mimi.
Aidha, amewataka wanaLongido kuendelza mapambano dhidi ya Rushwa na dawa za kulevya kwa kutambua rushwa nia adui wa haki na jukumu la kupambana na rushwa ni la kila mwananchi kuzuia Rushwa ni Jukumu lako na langu; tutimize wajibu wetu na kuongeza kuwa dawa za kulevya ni tatizo kwa afya ya binadamu huku vijana wengi wakitokomea epuka dawa za kulevya, zingatia utu, Boresha huduma za kinga na tiba.
Hata hivyo amesisitiza kuwa afya ya kila mtu inategemea lishe bora, kupitia Kauli mbiu ya Lishe sio kujaza tumbo, zingatia unachokula, hivyo ni vema kuzingatia lishe bora ili kuepuka magonjwa yasiyoambukiza ambayo yanaitesa jamii kwa sasa.
Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2024 ni "Tunza Mazingira, Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa Endelevu"
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.