Viongozi wa dini wameshauriwa kufanya kazi kwa bidii huku wakisimamia maadili ya utumishi wa Mungu.
Yamesemwa hayo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Idd Kimanta alipokuwa akishuhudia kuapishwa kwa askofu msaidizi wa kanisa la Free Pantegoste Church of Tanzania (FPCT).
Amewashauri viongozi hao wakawatumikie waumini wao kwa kuwajibika ili kujenga umoja na mshikamano wa kanisa hilo.
Kimanta amesema, hakuna maendeleo yanayoletwa bila kuwa na amani, umoja na mshikamano hivyo viongozi hao wapya wakadumishe hayo kwa ustawi wa Mkoa.
Askofu Mkuu wa kanisa la FPCT Robert Steven Mulenga,amewata viongozi hao wapya wakafanye kazi kwa ushirikiano wa karibu na viongozi wa serikali.
Akisoma historia fupi ya kanisa hilo askafu wa jimbo la Arusha Ayubu Muna amesema,kanisa hilo mpaka sasa limeshatimiza miaka 62 tokea kuanziashwa kwake Mkoani Arusha.
Hata hivyo kanisa hilo lina jumla ya matawi 361 kwa nchi nzima na zaidi ya waumini 20,000.
Kanisa la FPCT limewasimika viongozi wake katika nyazifa mbalimbali ili kuendelea kuliongoza kanisa hilo katika maadili na utaratibu wake.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.