Kamati ya Sheria ndogo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Abdallah Dadi Chikota (Mb), imewasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kukutana na Mwenyeji wake katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Albano Musa na kufanya kikao kifupi kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa leo tarehe 08 Februari, 2024.
Kamati hiyo ipo Mkoani Arusha kwa ziara ya siku moja ya mafunzo ya mfumo wa Manunuzi wa Serikali NeST yanayotolewa na Mamlaka ya usimamizi wa manunuzi ya Umma (PPRA) kwenye chuo cha ufundi Njiro.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.