Wajumbe wa Kamati ya siasa mkoa wa Arusha, wametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule Mpya ya sekondari Laja, kata ya Kansay, halmashauri ya wilaya ya Karatu, ikiwa ni ziara ya kawaida ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 - 2025
Ujenzi wa shule hiyo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 333.3, fedha kutoka Serikali Kuu, kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) chini ya miradi ya OPEC IV, ikiwa na lengo la kuboresha miundombinu ya elimu nchini ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki na wezeshi.
Mradi huo umetekelezwa kwa kushirikiana na wananchinwa kijiji cha Laja walio kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, ambapo wamechangia nguvu kazi kwa kusomba mchanga, mawe na kugonga kokoto, vyote vinathaminishwa kwa shilingi milioni 59.4.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.