Kamati ya Siasa mkoa wa Arusha, imetembelea na kukagua hali ya mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari Moivo kata ya Moivo, shule iliyojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 584.2, fedha kutoka Serikali Kuu kupitia miradi ya kuboresha miundombinu ya shule za sekondari nchini (SEQUIP).
Wajumbe wa Kamati hiyo, wametembelea mradi huo, ikiwa ni ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2020 -2025, kwenye halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru.
Wajumbe hao licha ya kuridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya CCM kupitia mradi huo, wameagiza kukamilisha mambo madogomadogo yaliyosalia, ikiwemo ukamilishaji wa miundombinu ya mifumo kwenye maabara, pamoja na samani kwenye maktaba na maabara za Sayansi na TEHAMA, ili kwa pamoja zianze kufanya kazi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Loy Thomas Sabaya, amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Arumeru kupitia mkurugenzi wa Hamashauri ya Arusha, kukamisha mambo yote kabla ya mwisho wa mwezi May 2024, kwa kukamilisha maabara na samani zote za maabara hizo.
Hata hivyo, ameipongeza Serikali kupitia halmashauri kwa ujenzi wa shule hiyo, shule ambayo licha ya kuondoa kero ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata elimu kwenye kata nyingine, imeongeza ari ya watoto kupenda shule na kutimiza azma ya Serikali ya kuhakikisha kila kata inakuwa na shule ya Sekondari ili watoto wanapate elimu kwenye mazingira karibu na nyumbani.
Awali mradi huo wa shule moya umetekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 584.2 ikijumuisha ujenzi wa Jengo la Utawala, vyumba 8 vya madarasa na ofisi, jengo la TEHQMA, Maabara za masomo ya Fizikia, Kemia na Baiolojia, vyoo vya wanafunzi pamoja ja kichomea taka.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.