Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda amehitimisha ziara yake ya Kikazi Wilayani Karatu kwa kufanya Mkutano Mkubwa wa Hadhara Karatu Mjini ambapo umati mkubwa wa Watu umempokea na kushiriki Mkutano wake uliokuwa na lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Mhe. Mkuu wa Mkoa amelazimika kuahidi kurejea tena Wilayani Karatu kutokana na matumaini makubwa ya wananchi kwa serikali yao pamoja na changamoto na kero nyingi ambazo ziliibuliwa kutoka kwa wananchi walioshiriki kwenye mkutano huo uliofanyika jioni ya leo Ijumaa Mei 24, 2024.
Salamu za Shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Mhe. Makonda kuwa Mkuu wao wa Mkoa zimetumwa kutoka kwa wananchi Mbalimbali wakionesha kuwa na matumaini makubwa ya kusikilizwa, kutatuliwa kero zao pamoja na kuharakishiwa maendeleo ya Wilaya yao iliyo Kitovu cha utalii mkoani Arusha.
#arushanautalii
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.