Katibu Tawala Mkoa wa arusha,Ndg.Richard Kwitega awaongoza Wakaazi wa Arusha katika maadhimisho ya siku ya Kisukari Duniani tarehe 14,Novemba,2017 katika Viwanja vya Makumbusho ya Azimio la Arusha
Katika hotuba yake, ndg.Kwitega aliwahasa Wakaazi wa Mkoa wa Arusha kuwa na tabia ya kupima afya zao mara kwa mara sambamba na kufanya mazoezi na kujiepusha na baadhi ya vyachakula ambavyo vinachangia ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya mwaka 2014,watu takribani 422 Duniani wanaugua ugonjwa wa kisukari, kati ya watu hao watu milioni 25 wanatoka bara la Afrika ambao ni nguvu kazi ya Taifa,na kueleza kuwa msingi mkuu wa maendeleo ya Taifa lolote Duniani ni afya ya watu wake,alieleza Kwitega.
"Lengo kuu la maadhimisho haya ya siku ya Kisukari Duniani ni kuendelea kukumbushana juu ya athari ya ugonjwa huu na kuhamasisha jamii kupima afya mara kwa mara ili kutambua mustakabari wa afya zetu,na endapo tukagundulika tumepata kisukari iwe rahisi kupata ushauri wa kitabibu namna ya kukabiliana nao". Aliongeza Kwitega
Naye,Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Dr. Wonanji alieleza kuwa katika kuhakisha elimu inawafikia wananchi, Ofisi yake ilitenga siku mbili za upimaji wa magonjwa ya kisukari na Shinikizo la Damu bure kwa vituo vinne(4) katika jiji la Arusha. Vituo hivyo ni Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mt.Meru, Kituo cha Afya Levolosi, eneo la Makumbusho ya azimio la arusha na kituo cha Ukumbi wa ABC, ambapo jumla ya waatu 1267 walipimwa kati yao wanaume walikuwa 649, na wanawake walikuwa 618. Watu 582 kati ya watu 1267 waligundulika kuwa na tatizo la shinikizo la damu na watu 84 waligundulika kuwa na tatizo la kisukari.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.