Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Paul Christian Makonda akiwa kwenye Kikao kazi na Maafisa wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Arusha, kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Jijiji la Arusha Aprili 20, 2024
Katika kikao Kazi hicho, Mhe. Makonda amelitaka Jeshi la Polisi Mkoani hapo, kuimarisha kitengo cha Intelejensia ili kuzuia na kudhibiti matukio ya uhalifu kabla hayajatokea madhara na athari kwa Jamii kuwa
wajibu wa msingi wa Jeshi la Polisi, kusimamia ulinzi na usalama wa wageni wa ndani na nje wanaoingia na kutoka mkoani humo
Mhe. Paul Makonda amewaeleza Maofisa hao wa Polisi kuwa wao ni watu muhimu katika kukuza Utalii mkoani Arusha na kuwataka kuhakikisha wageni na watalii wanakuwa salama kwenye shughuli zao mkoani hapa.
Amewasisitiza kuongeza kasi ya matumizi ya Teknolojia katika utekelezaji wa majukumu yake ili kuongeza ufanisi na kuchochea upatikanaji wa haki na weledi kwa wananchi huku akisistiza kuwa Teknolojia itarahisisha ufanyaji wa tathmini na ufuatiliaji wa matukio yanayofikishwa kwenye jeshi la Polisi.
Kwa upende mwingine Mhe. Makonda ametoa wito kwa wananchi kutoka ushirikiano kwa Jeshi hilo ili liweze litimiza majukumu yake na kuongeza kuwa ulinzi na usalama wa nchi unaanzia kwa mwananchi mwenyewe hivyo kila mwananchi anatakiwa kuwa mlinzi wake binafsi na mwenzake.
"Matumizi ya teknolojia kwa taasisi za haki jinai ni miongoni mwa mambo yaliyoelezwa na kutiwa msisitizo na Tume ya haki jinai iliyofanya uchunguzi na kuainisha mapungufu yanayokwamisha utendaji kazi, taasisi zote hizo ni muhimu katika upatikanaji wa Haki".Amesema Mhe. Makonda
Awali, Mkuu huyo wa Mkoa ameweka wazi kuwa, lengo la Kikao hicho ni kufahamiana na kujengeana uelewa wa pamoja kwa kuweka mikakati ya namna bora ya kuimarisha ulinzi na usalama kwenye mkoa wa Arusha na ameahidi kushirikiana na Jeshi hilo la Polisi.
.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.