Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Dr.Sophia Kashenge mapema Leo October 6 mwaka huu ameitambulisha Kampuni ya Pro Agro Grobla kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongela inayo jenga miundombinu ya Umwagiliaji katika mashamba ya Arusha Ngaramtoni pamoja na Tengeru.
Dr.Sophia amesema serikali ya Mkoa wa Arusha inapaswa kujua miradi yote inayotekelezwa na Wakala wa Mbegu za kilimo ASA katika Mkoa ilikuongeza usimamiaji na ufanisi wa kazi.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongela ameipongeza ASA kwa kuanza hatua nzuri za uwekaji wa Miundombinu ya Umwagiliaji katika mashamba yake ilikuwa na Uzalishaji wa Mbegu wa uhakika.
Mongela amempongeza Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe kwa kuonesha dira nzuri katika wizara ya kilimo na kuanza utekelezaji wa Bajeti hasa kwa kuanza na uwekaji wa Miundombinu ya Umwagiliaji.
Amsema kama Mkoa utahakikisha unatoa ushirikiano mkubwa katika kusimamia na kushauri Maendeleo ya Ujenzi wa Miundombinu hiyo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.