_____________________________
Na Mwandishi wetu.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Deogratius Ndejembi amekutana na kufanya kikao cha pamoja na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na kukagua maendeleo ya ukarabati wa uwanja wa Sheikh Amri jijini Arusha ambao maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi za mwaka huu zitafanyika.
Mhe Ndejembi ameelekeza kuwa hadi kufikia April 15, 2024 ukarabati wa uwanja uwe umekamilika lakini pia ameelekeza idadi ya mafundi kuongezwa ili kasi ya ujenzi iongezeke.
Kikao hiko kimehudhuriwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na wenye Ulemavu, Mhe Patrobas Katambi(MB), Katibu Mkuu wa Wizara, Mary Maganga pamoja na viongozi wa Shirikisho hilo wakiongozwa na Rais wao, Tumaini Nyamhokya
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.