Na Elinipa Lupembe
Loy Thomas Ole Sabaya ameshinda nafasi ya Uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha kwa kupata kura 463, kati ya kura 907 zilizopigwa na kuchukua nafasi ya Marehemu Zelothe Stephene Zelothe
Akitangaza matokea hayo, Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Antony John Mtaka, amesema kuwa, Ole Sabaya ameshinda uchaguzi huo kwa kupata kura 473, na kuwashinda wagombea wengine ambapo, Dkt.Daniel Mirisho Pallangyo amepata kura 374, Solomon Ole Sendeka Kivuyo kura 59 na kufauatiwa na Edna Israel Kivuyo, amepata kura10.
Kwa matokeo hayo, Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi, amemtangaza Loy Ole Sabaya, kuwa mshindi wa uchaguzi na kushika nafasi hiyo kwa kipindi kilichosalia Kikanuni.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.