Serikali imewataka Wasimamizi na Maafisa Rasilimali watu wa Sekta ya Umma na binafsi barani Afrika wazingatie swala la Utawala bora, utumishi wa umma wenye tija katika kusimamia rasilimali watu ili kutoa huduma bora na kudumisha Imani ya Wananchi kwa Serikali zao barani Afrika.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Haroun Ally Suleiman wakati akifunga Kongamano la 9 la Wasimamizi na Maafisa Raslimali Watu Barani Afrika kwenye Ukumbi wa mikutano ya kimataifa AICC, Mkoani Arusha, Novemba 06, 2024.
Waziri Haroun amesema kuwa, anaamini mbinu na maarifa waliyoyapata kwenye mkutano huo kuhusu mpango wa uwezeshaji, madaraka, uwajibikaji na uwazi katika Utumishi wa umma na maswala ya usimamizi wa rasilimali watu katika kukuza usimamizi utoaji huduma kupitia ushirikiano wa Sekta ya umma na binafsi utawezesha kutolewa huduma bora na kwa wakati, ukawawezesha kuzingatia na kutekelza masuala ya utawala bora katika maeneo yao ya kazi.
"Kauli Mbiu ya Utawala stahilivu na ubunifu katika kukuza Sekta ya Umma kupitia uongozi wa Raslimali watu, tunategemea ikalete mafanikio makubwa ya kijamii na kiuchumi kwenye maeneo yetu ya kazi". Amesema Mhe. Horoun
Amesisitiza kuwa, Mameneja na Maafisa Rasilimali watu hivyo waende wakazisaidie zisaidia Serikali zao kwenye maeneo muhimu waliyojengea uwezo kuhusua usimamizi raslimali watu Utawala imara,ubunifu na usimamizi wa hifadhi na kwa ajira endelevu zenye ushindani na mchakato wa ajira kwenye njia ya kidigitali katika Utumishi wa umma.
Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Rais wa Mtandano wa Mameneja Rasilimali watu Sekta ya Umma Afrika (APS- HRMnet) Xavery Daudi, amesema kuwa, wamepata fursa ya kujadili changamoto wanazokutana nazo na namna ya kuzitatua na kusisitiza, Uongozi unaendelea kuhamasisha usitawi wa Jumuiya hiyo barani Afrika.
Ameweka wazi kuwa, lengo la Kongamano hilo la siku tatu lilikuwa ni kuwawezesha Wasimamizi na Maafisa Rasilimali watu hao, kutoka nchi wanachama kubadilisha uzoefu, kujifunza na kupata uelewa mpana na mwelekeo wa kidunia katika usimamizi wa raslimali watu na maendeleo makubwa ya kiteknolojia yanayoshuhudiwa kupitia mawasiliano.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.