Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella amekabidhi Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe.Ally Hapi.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zikiwa Mkoani Arusha zimetembelea, kukagua na kuweka mawe ya msingi miradi 60 yenye thamani ya sh. bilioni 26.8 ambapo miradi 11 iliwekewa mawe ya msingi,miradi 20 ilizinduliwa, miradi 3 ilifunguliwa na miradi 26 ilitembelewa na kukaguliwa.
Mwenge wa Uhuru ulipokelewa Mkoani Arusha Juni 20 kutoka Mkoa wa Manyara na Juni 27 umekabidhiwa Mkoani Mara.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.