Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amewasili mkoani Arusha na Kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Babu, kwa ndege ya shirika la ndege Tanzania, kwenye uwanja wa Kimataifa Kilimanjaro, mchana wa leo Februari 09, 2024.
Makamu wa Rais ameambata na Mkwewe Bi. Mboni Mpango, kwa ziara ya siku mbili mkoani Arusha.
Akiwa mkoani Arusha, Makamu wa Rais, atakwenda wilaya ya Longido Tarafa ya Ketumbeine na kuzindua Kituo cha Afya Kitumbeine, Kuwasha Umeme wa REA katani hapo pamoja na kufanya Mkutano wa Hadhara na wananchi wa Ketumbeine.
Mhe. Dkt. Mpango ataweka jiwe la Msingi katika shule mpya maalum ya wasichana 'Longido Samia Suluhu Girl's Secondary School' eneo la Orbomba na Kufanya mkutano wa Hadhara kijiji cha Oltepes.
Siku ya pili ya ziara yake, Makamu wa Rais ya tarehe 11 Februari 2024, atashiri Ibada ya Kumuweka Wakfu na kuwaingiza Kazini Askofu Mteule Dkt. Godson Abel Mollel
na Msaidizi wa Askofu Mchg. Laretoni Loishiye Lukumay , Dayosisi ya Kaskazini Kati, Usharika wa Kimandolu Jiji la Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.