Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amesisitiza umuhimu wa viongozi wa dini kuzingatia masomo ya dini kwenye ngazi mbalimbali za Elimu kwenye maeneo yao ya kiuongozi kwa kuhakikisha shule zote zinakuwa na waalimu wa dini waliobobea.
Makamu wa Rais ametoa wito huo leo Jumamosi Septemba 21, 2024 wakati alipokuwa akihitimisha Kongamano la nne la Uhuru wa Kidini barani Afrika kwenye Viwanja vya michezo vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha lililokuwa na kaulimbiu isemayo "Kuishi pamoja kwa amani barani Afrika, Tunu isiyopingika ya dhamiri ya binadamu."
Kauli ya Makamu wa Rais imekuja baada ya Ombi la Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda kwa Viongozi wa dini, akitaka Morali zaidi kwa Viongozi wa dini katika kutafuta na kuwapanga waalimu wa dini kwenye shule zinazopatikana Mkoani Arusha ili kusaidia katika kukuza maadili mema kwa watoto.
"Nimefanya utafiti katika mkoa wetu,tuna vipindi viwili kwa kila wiki, karibia karibia dakika 80 kwa wiki zilizotengwa kwaajili ya kuwafundisha watoto wetu habari za Mungu lakini moja ya changamoto kubwa tuliyoipata ni kuwa hakuna waalimu wa kufundisha watoto wetu habari za Mungu." Amesema Mhe. Makonda.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.