Na Elinipa Lupembe
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi - CCM Mkoa wa Arusha, Loy Ole Sabaya, amesema kuwa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 ni muhimu kwa Mipango cha Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha na Taifa.
Mwenyekiti Sabaya, amesema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2022 kwa viongozi wa makundi mbalimbali ya kijamii, mkoa wa Arusha, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa AIM MALL Jijini Arusha leo tarehe 11 Desemba, 2023.
Amesisitiza kuwa, licha ya kuwa Sensa ni muhimu kwa Taifa lakini Matumizi ya Takwimu za matokeo ndio muhimu zaidi na kuwataka washiriki wote kuzingatia maelekezo, yatakayotolewa na wawezeshaji wa Mafunzo hayo, ili yaweze kuwasiadia namna bora ya matumizi ya Takwimu za matokeo ya Sensa ya Watu ma Makazi ya mwaka 2022.
Adha, amebainisha kuwa, wao kama viongozi wa chama, matokeo hayo ya Sensa, ni muhimu katika kupanga mipango, kufanya ufuatiliaji pamoja na kufanya tahmini katika mchakato mzima wa utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha na Taifa.
"Sisi kama viongozi ambao ni wawakilishi wa wananchi, tuko tayari kupokea mafunzo haya muhimu kwetu na nchi yetu, tufundishwe ili itusaidie katika matumizi yetu ya kikazi, tunaamini yatatusaidi katika mkoa na wilaya zetu, mkoa na Taifa" Ameweka wazi Mwenyekiti Sabaya.
Hata hivyo, Ole Sabaya, ukiwa ni mkutano wake wa kwanza tangu achaguliwe kushika nafasi hiyo, ametumia fursa hiyo, kuwamewashukuru wajumbe wote kwa kumchagua na kumpa dhamana ya kuwahudumia wanaArusha na ameahidi kufanya kazi hiyo kwa uadilifu kama walivyomuamini.
Mkutano huo umefunguliwa na Katibu Tawala Msaidizi Utumishi na Rasilimali Watu, mkoa wa Arusha, David Lyamongi kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha, ukiwa na lengo la kuyajengea uwezo makundi mbalimbali ya kijamii juu ya matumizi sahihi ya matokeo ya Sensa ya watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2022.
Makundi hayo ni pamoja na watalamu wa Mkoa na Serikali za Mamlaka ya Serikali za Mitaa, viongozi wawakilishi wa wananchi, viongozi wa Siasa, dini na mila, Watendaji wa mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, watendaji wa kata, kamati ya Sensa Mkoa pamoja na wawakilishi wa makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo watu wenye mahitaji maalum.
#arushafursalukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.