Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Arusha utakimbizwa umbali wa Kilomita 1168.47 na Miradi 62 yenye thamani ya sh. 47,290,543,421.83 itapitiwa na Mwenge wa Uhuru 2023, ambapo sh.31,184,729,891.22 nikutoka Serikali kuu, sh.1,657,992,282.09 halmashauri, sh.3,297,238,870.52 wahisani na sh. 11,150,582,378.00 wananchi.
Katika Miradi hiyo, 16 itawekewa mawe ya Msingi yenye thamani ya sh. 26,941,819,117.51.Miradi 14 itazinduliwa yenye thamani ya sh.11,206,373,826.32,miradi 8 itafunguliwa kwa thamani ya sh. 694,994,000.00 na miradi 24 itatembelewa na kukaguliwa kwa thamani ya sh. 8,457,506,478.83.
Mwenge wa Uhuru 2023,umepokelewa Wilayani Longido ukitokea Mkoa wa Kilimanjaro na utakimbizwa katika halmashauri zote za Mkoa wa Arusha na utakabidhiwa Mkoani Mara ukitokea Wilaya ya Ngorongoro.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.