Mfumo wa Kielektoniki wa Usimamizi wa Utendaji Kazi (PERMIS&PIMIS) na Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimali Watu ( HR Assesment) umezinduliwa rasmi katika mkoa wa Arusha kwa wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi za Serikali zenye makao yake makuu Arusha, kupatiwa mafunzo yaliyofanyika, kwenye ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa mkoa Arusha.
Akifungua mafunzo hayo, Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Missaile Albano Musa, amewataka wakurugenzi wote, kusimamia watalamu waliochini yao, katika zoezi zima la ujazaji wa taarifa sahihi zinazohitajikwa kwenye mfumo huo kwa kuzingatia muda uliopangwa kabla ya tarehe 31 Desemba, 2023.
Amebainisha kuwa mfumo huo kwa ilivyoelekezwa na serikali ni muhimu katika utekelzaji wa majukumu ya mtumishi yatakayozingatia kujituma, weledi na uwajibikaji unayoendana na malengo yaliyowekwa kulingana na cheo, nafasi na taaluma ya mtumishi, kuelekea kufikia lengo la taasisi na serikali kwaujumla.
"Mfumo huu kama tulivyojifunza uko wazi, utakaofanya upimaji bila upendeleo, kila mtumishi atalazika kuwajibika huku mfumo ukimpima na kumfanyia tathmini kazi ambayo ilifanywa kianalojia na kusababisha uzembe na malalamiko kati ya mpimaji na mpimwaji, mfumo huu utaondoa utata huo" Amesema Afisa Tawala huyo
Akiwasilisha malengo ya mifumo hiyo, Mkurugenzi, Idara ya Utumishi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, amesema kuwa, Mfumo huo mpya umekuja kutatua changamoto za mifumo iliyotangulia, ambayo licha ya kuwa mifumo hiyo ilikuwa haisomani lakini ililalamikiwa kuto kutenda haki kwa watumishi kwa kuwa, hakuwezesha upimaji wa wakati na kushindwa kutoa tahmini ya utendaji kazi wa kila siku wa mtumishi, huku ukiacha mbali tahmini ya Taasisi.
"Mifumo hii ni rafiki kwa mtumishi, ikimpa nafasi ya kupimika utendaji kazi wake wa kila siku na kutoa matokeo bila upendeleo ikiwa na vigezo vya upimaji vinavyozingatia majukumu ya kila mtumishi kulingana na cheo na majukumu yake"
Awali, mfumo huo mpya maalumu, kwa ajili ya kufanya tathimini ya hali ya watumishi wa Umma kwa uwazi na kuondokana na changamoto za mifumo iliyotumika hapo awali
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.