@ortamisemi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewaelekeza viongozi wa Halmashauri ya Arusha kupitia Mkuu wa wilaya ya Arumeru na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha, kuzingatia vigezo vilivyowekwa kisheria ili kupandisha hadhi Mamlaka ya Mji mdogo kuwa Mamlaka ya Mji.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi kwenye Halmashauri hiyo ya kukagua shuguli za utekzlzaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na viongozi na wannachi wa halmashauri hiyo Oktoba 02, 2024.
Amesema, "Nimepokea ombi lenu la kutaka kuanzisha Mamlaka ya Mji na hatimaye kuwa na Manispaa huko mbeleni lakini ninachoweza kuwashauri kwa sasa ni kuwa zingatieni vigezo na sifa za Halmashauri ya Mji na mkijitathimini kama mmekidhi wasilisheni mapendekezo hayo Ofisi ya Rais -TAMISEMI kwa ajili ya hatua zaidi"
“Kuwa na mamlaka ya mji mdogo sio kitu ninachopendekeza sana kwa sababu kwanza inahitaji kulelewa na Halmashauri ya Wilaya hivyo katika mapato yenu mtatoa fedha kwa ajili ya kuendesha mamlaka ya mji mdogo na kwenda kuwa Manispaa mtakua mmevuka hatua ya kuwa Mamlaka ya Mji kama mnadhani mna sifa hizo wasilisheni maombi yenu yakiwa yamepita kwenye vikao vyote muhimu na yakifika Ofisi ya Rais - TAMISEMI tutayachambua kama mmekidhi vigezo mtapa hadhi ya Mji, »amesema.
Aidha ameongeza kuwa changamoto zilizowasilishwa amezipokea hususan ikiwamo ya miundombinu ya barabara za lami na kuahidi kufanyia kazi.
Waziri Mchengerwa yupo kwenye ziara ya Kikazi mkoani Arusha na atatembelea Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Meru pamoja na Jiji la Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.