Na Elinipa Lupembe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwatunuku Maafisa Wanafunzi 62 wa Kundi la 04/ 20 Shahada ya Sayansi ya Kijeshi ya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi(TMA) Monduli Mkoani Arusha katika Mahafali ya nne tarehe 18 Novemba 2023 pamoja na kuwapa zawadi kwa Maafisa wanafunzi wawili, waliofanya vizuri zaidi kwa kundi hilo.
Maafisa Wanafunzi hao wamekuwa Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambao Maafisa wapya kundi la 04/20 - BMC ni 62 wamepata mafunzo katika chuo hicho kwa muda wa miaka mitatu na kuhitimu Shahada ya Sayansi ya KKijeshi
"Nimetunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi Kundi la 04/20 - Shahada ya Sayansi ya Kijeshi na Kundi la 70/22 (Regular) kwa Cheo cha Luteni Usu"
Aidha Amiri Jeshi Mkuu, amebainisha kufarijika zaidi kwa kuona Jeshi la Wanachi Tanzania, likiendelea kupiga hatua kubwa za kimaendeleo na uwekezaji katika Taaluma ya Sayansi ya Kijeshi pamoja na Rasilimali watu.
"Weledi, nidhamu, uzalendo, unaongezeka siku hadi siku zinatupeleka katika hatua bora zaidi kwa faida ya Taifa letu tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Wananchi Tanzania tarehe 01 Septemba, 1964, ni faraja na fahari kwa nchi yetu" Ameweka wazi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan
Kabla ya kutunuku mafunzo hayo, Mhe. Rais amekagua gwaride la heshima, lililoandaliwa na Maafisa Wanafunzi hao kutokana na Maelekezo ya Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Brigedia Jenerali Jackson Jairos Mwaseba na kusimamiwa na Mkufunzi Mkuu Kanali Nilinda William Duguza.
Hata hivyo Mkuu huyo wa chuo, alitoa taarifa fupi ya mafunzo ya Maafisa hao wapya, amesema kuwa, chuo kinajivunia kwa mara ya kwanza kimewezesha mafunzo ya Shahada hiyo kwa kujisimamia pasipo ushirikiano wa kimafunzo na chuo cha Uhasibu Arusha IAA kama ilivyokuwa hapo awali
Awali sherehe hizo za Maafali zilimefanyika kwenye Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (Tanzania Millitary Academy – TMA) Mkoani Arusha, zikihudhuriwa na vongozi mbalimbali wa Kijeshi, viongozi wa Chama na Serikali, wageni waalikwa ndani na nje ya nchi, zilizosheheni burudani zilizowavutia watu wote.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.