Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika kongamano la 16 la Ununuzi wa Umma, nchi za Jumuia ya Afrika ya Mashari, litakalokutanisha wataalam wa maswala ya manunuzi ya Umma na Ugavi, Kongamano litakalonza Jumatatu Septemba 09, 2024 Mkoani Arusha.
Kongamano hilo la siku nne kuanzia tarehe 09 mpaka 12 Septemba, 2024, litafanyika kwenye Kituo cha Mikutano ya kimataifa Arusha - AICC, ukumbi wa likikutanisha Wataalam wa Manunuzi ya Umma na Ugavi kutoka nchi zote saba za Jumuia ya Afrika Mashariki.
Mkutano huo wenye lengo kujadili fursa za kidigitali katika sekta ya manunuzi ya umma, kuhikiza matumizi ya mifumo ya manunu, kubadilishana uzoefu pamoja na kujadili changamoto zinazoikabili sekta hiyo na kupeana mbinu na mikakati ya kukabiliana na kutatua changamoto hizo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.