Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili mkoani Arusha jioni ya leo, kupitia Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ndege ya shirika la ndege Tanzania na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K.Mongella na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu, tarehe 17 Novemba, 2023.
Akiwa mkoani Arusha, Mhe. Rais anatarajia kuwatunukia Kamisheni Wanajeshi katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) kilichopo wilayani Monduli, mkoa wa Arusha.
#karibuarushamama karibuArushamama
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.