Na Elinipa Lupembe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Jeshi 575 kwa kundi la 04/20 -Shahada ya Sayansi ya Kijeshi (BMS) na Kundi 70/22 - Regular kwa cheo cha Luten Usu katika chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli leo tarehe 18.11.2023.
Maafisa Wanafunzi hao wamekuwa Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambao Maafisa wapya kundi la 04/20 - BMC ni 62 wamepata mafunzo katika chuo hicho kwa muda wa miaka mitatu na kuhitimu Shahada ya Sayansi ya Kijeshi.
Kundi jingine la wahitimu 447 ni kundi la 70/22 - Regular ambao wamepata mafunzo yao kwa muda wa mwaka mmoja huku Maafisa wanafunzi 66 wakipata mafunzo ya Urubani kutoka nchi rafiki.
Awali kabia ya kutunuku mafunzo hayo, Mhe. Rais amekagua gwaride lililoandaliwa na Maafisa Wanafunzi hao kutokana na Maelekezo ya Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Brigedia Jenerali Jackson Jairos Mwaseba na kusimamiwa na Mkufunzi Mkuu Kanali Nilinda William Duguza.
Katika hafla hiyo Mhe. Rais alitoa zawadi kwa Maafisa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kwa makundi yote mawili pamoja na kumvisha Nishani Afisa Mwanafunzi Rubani kwa niaba ya wenzwenzi
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.