Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu hassan, imeendelea kutekeleza mpango wa kunusuru kaya masikini mradi unaoteklezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 981.3 kwa walengwa walio kwenye mpngo huo, Mkoa wa Arusha.
Akizungumzia na mwandishi wa habari hizi, Mratibu wa TASAF Mkoa wa Arusha, Richard Nkini amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kimetolewa kwa kaya 41,272 ikiwa ni ruzuku ya mwezi Julai na Agosti 2024 kwa halmashauri zote saba za mkoa wa Arusha.
Amefafanua kuwa, fedha hizo ni mahsusi kwaajili ya ruzuku ya Msingi, Elimu pamoja na afya ili kuhakikisha walengwa hao wanapata mahitaji yao ya msingi ikiwa ni pamoja na watoto wa kaya hizo kupata mahitaji muhimu ya kuwawezesha kuhudhuria masomo na kliniki kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.
Fedha hizi licha ya kuwasaidia walengwa kuapata mahitaji ya familia lakini zaidi zinawawezesha kuanzisha miradi midogo midogo ya kuinua pato la familia na hatimaye kutoka kwenye lindi la umasikini uliokithiri". Amesema Nkini.
Hata hivyo wanufaika hao wameishukuru Serikali yao ya awamu ya tano, kwa kuendelea kuwajali wananchi wa kipato cha chini, kwa kuwa kabla ya kuwepo kwa mradi huo wengi walishindwa kuendesha maisha yao na familia zao, kutokana na hali ngumu maisha iliyosababishwa na kipato duni.
Mmoja wa wanufaika hao, Bibi Zuhura Ally ambaye ni mkazi wa Kata ya Ngarenaro amesema kupitia fedha hizo, anamudu kuwasomesha wajukuu wake ambao ni yatima kwa kuwnunulia mahitaji ya shule matumizi huku akutumia fedha nyingine kwa matumizi ya familia, jambo ambalo hapo awali ilikuwa ni ngumu kwake na familia.
Ninaishukuru Serikali kwa kutujali, mimi ninalea wajukuu zangu ambao ni yatima, ninamshukuri Mungu, huu mradi wa TASAF umetusaidia wengi, kabla ya hapo tulikuwa na hali ngumu ya maisha". Amesema Bibi Zuhura.
Ikumbukwe kuwa, mradi wa Kunusuru kaya Masikini nchini ni utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.