Na Elinipa Lupembe
Kamishna msaidizi wa Ardhi mkoa wa Arusha Geofrey Mwamsojo leo, amemkabidhi hati ya kiwanja mama mjane Bi. Arafa Mohammed mkazi wa Olematejoo, jijini Arusha leo Apili 25,2024
Mjane Arafa ambaye aliwasilisha malalamiko yake kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Mhe. Jerry Silaa alipofanya Kliniki ya ardhi Jijini Arusha na hatimaye kuagiza kurejeshewa eneo lake hili ambalo anamiliki kihahali na kutengenezewa hati.
Awali, Arafa ameweka wazi kuwa, eneo hilo lilidhulumiwa na Bw. Alex Mtinange, na kuhangaika kutafuta haki yake kwa takribani miaka 15 na hatimaye, Waziri wa Ardhi kupitia Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Arusha amefanikiwa kurejeshewa eneo hilo na leo kukabidhiwa hati miliki.
"Ninaishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kuwahudhumia wananchu hasa sisi wanyonge, namshukurj Waziri wa Ardhi Mhe. Jerry Silaa kwa kusimamia kupatikana ka eneo langu zaidi ninamshukuru Kamishna wa ardhi na timu yake, wamepambana na kuhakikiha nimepata hati ya eneo langu" Amesema Arafa
Inqsemekana kuwa, jitihada za mama huyo ziligonga mwamba, hadi jambo hilo lilipotua kwenye meza ya Waziri Silaa aliyetoa maelekezo kwa Kamishna msaidizi wa Ardhi mkoa wa Arusha kufuatilia na kuhakikisha mama huyo anapata haki yake, jambo ambalo limefanikiwa, ingawa nyumba iliyokuwa imejengwa ilikuwa imebomolewa na hivyo kubaki kiwanja pekee
Naye Kamishna wa Ardhi mkoa wa Arusha, Geofray Mwamsojo amesema mama huyo aliwasilisha malalamiko yake kwa Waziri wa Ardhi, ambapo alieleza marehemu mume wake alijenga nyumba kwenye kiwanja hicho na walikuwa wakiishi wote kama familia lakini baada ya mume wake kufariki, mwaka 2012, Bwana Alex Mtinange, ambaye inatajwa kuwa alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na binti yake alijaribu kudhulumu eneo hilo.
Baada ya kugundua eneo hilo na familia ya mama Arafa aliloachiwa na Marehemu mume wake, Waziri aliamuru kurejeshewa eneo hilo na tayari ametengenezewa hati miliki na kukabidhiwa mapeme leo.
@maelezonews @ikulu_mawasiliano @ortamisemi @wizara_ya_ardhi @baba_keagan
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.